Klabu ya Young Africans inatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa kawaida Juni 24 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Convention uliopo Posta, Dar es salaam.

Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo na kusainiwa na Rais wa klabu hiyo, Hersi Said inasema kwa mujibu wa ibara ya 20 ya Katiba ya Young Africans anapenda kuwatangazia wanachama Mkutano Mkuu wa kawaida.

Taarifa hiyo imetaja ajenda 11 ambazo zitakajadiliwa katika mkutano huo ambapo ni kufungua mkutano, uhakiki wa wajumbe waliohudhuria mkutano huo, kuthibitisha ajenda, kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliopita.

Ajenda nyingine ni yatakanayo na kumbukumbu za mkutano uliopita, hotuba ya Rais, kupokea na kujadili taarifa za kazi kutoka kwa Kamati ya Utendaji, kuthibitisha hesabu zilizokaguliwa za mwaka uliotangulia pamoja na kusomewa mapato na matumizi ya klabu.

Aidha mkutano huo utathibitisha bajeti kwa mwaka unaofuata, kuthibitisha wajumbe wa baraza la wadhamini na kufunga mkutano.

Huu utakuwa mkutano wa kwanza tangu uongozi wa Hersi kuingia madarakani Julai mwaka jana.

Joao Cancelo awekwa sokoni kwa bei punguzo
Wananchi wahimizwa ushiriki mchakato Katiba mpya