Kikosi cha Young Africans kesho Jumamosi, kitashuka kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam kumenyana na Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara, katika kindumbwe Ndumbwe cha Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo utakua muhimu kwa pande zote mbili, kulingana na nafasi zao kwenye msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara, ambapo kwa upande wa Young Africans wanahitaji kuutumia mchezo huo kuendelea kupambana kwenye vita ya kuiwania nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wakitanguliwa na Azam FC, kwa tofauti ya alama moja.

Azam FC inashika nafasi ya pili kwa kufikisha alama 58, Young Africans ipo nafasi ya tatu kwa kumiliki alama 57.

Ndanda watahitaji kuutumia mchezo huo kuendelea kujiimarisha katika mapambano ya kukwepa kushuka daraja msimu huu 2019/20, kwani mpaka sasa wameshakusanya alama 35, zinazowaweka kwenye nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa kuhakikisha mpango wa kupata alama tatu muhimu unakamilika, Wachezaji wa Young Africans jana Alkhamis walifanya kikao na kuweka mkakati wa kupata ushindi kwenye mchezo huo na mingine yote iliyobaki.

Baada ya Simba kujihakikishia ubingwa, Young Africans wanahitaji kumaliza msimu kwa heshima, angalau kumaliza katika nafasi ya pili.

Hesabu kali wamezihamishia kwenye michuano ya kombe la FA ambayo wanahitaji kushinda ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao.

Jumanne Juni 30, Young Africans watachuana na Kagera Sugar katika mchezo wa Robo Fainali ambao utapigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

Michezo mingine itakayochezwa mwishoni mwa juma hili.

Serikali yazitaka shule binafsi kupokea wanafunzi
Serikali yaboresha upatikanaji maji, Bukoba