Uongozi wa klabu ya Young Africans umelaani vikali vitendo vya uvunjivu wa amani vilivyotokea katika mchezo wao dhidi ya GD Sagrada Esperanca vilivyofanywa na mwamuzi wa mechi hiyo na vyombo vya usalama.

Katika mchezo huo Young Africans walifanyiwa vurugu ikiwemo na golikipa wa timu hiyo Deogratius Munish ‘dida’ kupigwa na mawe na Polisi kuingia uwanjani mara kwa mara.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Young Africans, Jerry Muro amesema kuwa Mwamuzi wa mchezo amefanya vitendo vingi ambavyo havipo katika sheria 17 za soka.

“Mwamuzi amefanya vitendo vingi vya uvunjivu wa sheria za mpira wa miguu ikiwemo kuwatoa wachezaji mchezoni kwa kuwapatia kadi huku upande mwingine wakiwa wanafanya makosa pasi kupatiwa onyo lolote,”amesema Muro. Kwa sasa uongozi umeamua kuandika barua kwa shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) kuomba kuondolewa kwa mwamuzi huyo ikiwemo kufungiwa au kutokuchezesha  mechi zao.

Muro amesema kikosi kipo nchini Afrika kusini kikisubiri ndege ya kesho saa 4asubuhi na kuingia mchana ambapo wataingia kambini moja kwa moja kwa ajili ya safari kuelekea Songea kumalizia mchezo wao dhidi ya Majimaji utakaopigwa Jumapili.

TFF Wachimba Mkwara Mzito Kuelekea Michezo Ya Mwisho Ya Ligi
La Liga Kuzibana Vikali Klabu Za Nchini Hispania Kuanzia 2016-17