Klabu ya Young Africans imekanusha taarifa za kuhusika na mpango wa kutuma ofa ya kumsajili kiungo wa Azam FC Aboubakari Salum “Sureboy”, katika kipindi hiki cha dirisha la usajili.

Young Africans imekua ikihusishwa na mipango wa kumsajili kiungo huyo mara kwa mara, huku ikidaiwa mchezaji huyo ana mapenzi na klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Sureboy mwenye umri wa miaka 28 amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC, na huenda akaongeza mkataba wa muda mrefu zaidi na ikiwezekana wa maisha ndani ya klabu hiyo.

Hata hivyo uongozi wa Azam FC upo tayari kumuachia Sureboy kama atahitaji kuondoka, endapo watapata ofa itakayowaridhisha kutoka kwenye klabu yoyote yenye lengo la kumsajili.

Sureboy ameicheza timu ya taifa (Taifa Stars) michezo 42 na kufunga bao moja.

Ajira: Nafasi za kazi kwa watangazaji, waandishi wa habari
Mwantika kuachana na Azam FC