Winger wa kutoka nchini Niger Issoufou Boubacar Garbar ambaye alisajiliwa na klabu ya Young Africans wakati wa dirisha dogo la usajili la mwezi January mwaka huu, amepewa barua ya kuvunjiwa mkataba na klabu hiyo.

Garbar ameshindwa kudhihirisha ubora wake kwenye kikosi cha Young Africans kwa kushindwa kupambana na kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza, na mara nyingi amekuwa akianzia kwenye benchi huku akianzishwa kwenye michezo pekee.

Mniger huyo amedumu kwa muda wa miezi minne tu tangu aliposajiliwa na mabingwa hao wa VPL na kombe la shirikisho katika msimu wa 2015-16 uliomalizika mwezi uliopita.

Wakati huo huo uongozi wa klabu ya Young Africans, umemsainisha mkataba mpya mchezaji wake ‘kiraka’ Mbuyu Twite.

Mbuyu Twite

Twite amesainishwa mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo, baada ya taarifa ambazo hazikua rasmi kusambaa katika mitandao ya kijamii zikidai, tayari alikua ameshatemwa.

Nyota huyo amekuwa kwenye wakati mgumu wa kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara.

Stephen Okechukwu Keshi Amefariki Dunia
Zitto Kabwe aingia Mikononi mwa Polisi