Uongozi wa klabu ya Young Africans rasmi umepeleka malalamiko Shirikisho la soka nchini (TFF) kuhusu kushawishiwa kwa winga wake Bernard Morrison kujiunga na klabu nyingine kinyume Cha sheria, ili haki itendeke na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Kaimu katibu Mkuu wa Young Africans Wakili Simon Patrick amesema klabu haiwezi kufumbia macho maelezo yaliyotolewa na Winga huyo ambaye ameweka wazi kila kilichotokea.

“Mchezaji wetu ameeleza kila kitu,hivyo tumepeleka malalamiko yetu TFF na chombo husika kitasikiliza kutokana na ushahidi tuliouwasilisha na kutolea maamuzi.”

Patrick amesema tayari ushahidi umekusanywa kwa ajili ya suala hilo ikiwa ni pamoja na kumhoji mchezaji na vielelezo vingine vinavyohusiana na suala hilo.

Wakati huo huo Afisa Habari wa Young Africans Hassan Bumbuli amesisitiza kupelekwa kwa malalamiko kwenye Shirikisho la soka nchini (TFF) kuhusu kushawishiwa kwa Bernard Morrison kujiunga na klabu nyingine kinyume Cha sheria.

“Ni kweli tumepeleka malalamiko yetu TFF kuhusu suala la wao kutaka kumrubuni Morrison, hatukurupuki, tuna ushahidi wa kutosha.” Amesema Bumbuli.

Hata hivyo Bumbuli hakusema alikua anailenga klabu gani ambayo wana ushahidi ilitaka kumrubuni mchezaji huyo kutoka Ghana.

Simba SC imekua ikituhumiwa kufanya mchezo huo mchafu, japo Afisa mtendaji wake (C.E.O) Senzo Mbatta Mazingiza amekua kikanusha klabu hiyo kuhusika.

Breaking News: Rais Magufuli atengua uteuzi wa watatu Arusha, amuondoa Mrisho Gambo
Elma Aveiro amshambuliaji Sarri