Kocha Mkuu wa Young Africans, Cedric Kaze amesema kikosi chake kitaingia tofauti katika mchezo wa mzunguko wa nne wa michuano ya Kombe la FA ‘ASFC’ dhidi ya Kengold ili kujihakikishia ushindi mnono na kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Young Africans watakua wenyeji wa mchezo huo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam, huku ukiwa mchezo wao wa kwanza wa michuano hiyo kwa msimu huu, baada ya kupita kwa kupewa mabao matatu dhidi ya Singida United iliyoshishwa daraja na Shir5ikisho la soka nchini ‘TFF’.

“Tunajua mechi hiyo ni sawa na fainali, kwa sababu ili uendelee na mashindano ni lazima ushinde, tunataka kuwapa furaha mashabiki wetu, tumejipanga na tunaendelea kujiimarisha kuelekea mechi hiyo muhimu,” Amesema Kaze.

Kocha huyo kutoka nchini Burundi amesema wachezaji wake waliokuwa majeruhi akiwamo kiungo Mkongomani Mukoko Tonombe hali yake imeimarika na yuko tayari kuitumikia Young Africans.

Wakti huo huo daktari wa Young Africans Nahumu Muganda amethibitisha taarifa za kupona kwa mshambuliaji kutoka nchini Burkina Faso Yacoba Sogne ambaye alikua majeruhi tangu mwezi uliopita.

Muganda amesema: “Yacouba amepona na sasa yupo fiti kuanza kuichezea Yanga katika michezo ijayo ya ligi na mashindano mengine tunayoshiriki katika msimu huu.

“Jumatatu alianza mazoezi ya pamoja na timu, mara baada ya timu kurejea kambini baada ya mapumziko ya siku moja waliyopewa wachezaji.

“Tulikuwa na majeruhi saba pamoja na Mukoko (Tonombe) ambaye yeye aliumia mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Kabwili na Ninja ambao wenyewe wamepona wamerejea uwanjani, hivyo wamebakia watatu pekee ambao ni Said Ntibazonkiza, Dickson Job na Balama Mapinduzi.”

Magufuli: Ilala mnastahili kuwa Jiji, hamjapendelewa
Manara, Magori wamkali kooni Senzo