Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Cedric Kaze, amesema wapo tayari kwa mchezo wa kesho Jumamosi (Novemba 26), dhidi ya Mbeya City FC.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23, umepangwa kuanza kurindima majira ya saa moja usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku Young Africans ikisaka kuendeleza Rekodi ya kutofungwa mchezo wa 49, na Mbeya City FC ikidhamiria kusitisha Rekodi hiyo.

Kaze amezungumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa (Novemba 25) majira ya Mchana jijini Dar es salaam, ambapo amesema kikosi chao kipo tayari kwa mchezo huo, baada ya kufanya maandalizi kabambe, ambayo wanaamini yatawabeba na kufikia lengo la kupata alama tatu muhimu.

“Tumejiandaa vizuri kwa sababu tunajua Mbeya City mechi zao za karibuni wamefanya vizuri. Hatuna rekodi nzuri nao mchezo uliopita kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Ni timu ambayo imekuwa ikitupa changamoto ambayo tumejiandaa kuikabili”

“Ni kweli tuna takwimu nzuri ambayo ni heshima kwa Klabu. Lakini hatuchezi kwa sababu ya rekodi ya unbeaten, tunacheza kushinda ili tufikie malengo yetu. Kwenye mafanikio yetu hatuna malengo ya unbeaten, tuna malengo ya kutwaa mataji yaliyopo mbele yetu. Unbeaten ni matokeo sio mafanikio. Sisi tunataka mafanikio”

“Aziz Ki na Djigui Diarra wamerejea kutoka kwenye majukumu ya timu zao za Taifa. Vile vile Yannick Bangala amerejea baada ya kumaliza adhabu yake ya kadi tatu za njano” Cedric Kaze kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya City.” amesema Kocha Cedric Kaze

Hadi sasa Young Africans inaongoza Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 29 sawa na Azam FC inayoshika nafasi ya Pili, huku Mbeya City FC yenye alama 19 ikishika nafasi ya Sita.

DAWASA yatakiwa kuimarisha miundombinu
TBS yawataka wafanyabiashara kushirikiana na taasisi za serikali