Rais wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Injinia Hersi Said amesema klabu hiyo haikukurupuka kusiani Mkataba na Kampuni ya Haier, kama inavyoelezwa, baada ya Wadhamini wao SportPesa kutoa taarifa jana Jumatano (Februari Mosi).

Young Africans ilisaini mkataba kampuni ya Haier wenye thamani ya Tsh bilion 1.5, Jumatatu (Januari 30), jijini Dar es saaam, hatua ambayo inapingwa na SportPesa kwa madai ya Mkataba wao kukiukwa.

Akizungumza mapema leo Alhamis (Februari 02) kupitia Kipindi cha Sports HQ cha EFM Radio, Hersi amesema: “Tuna majadiliano ya kina na SportPesa ambao ndiyo wadhamini wetu wakuu. Young Africans inafuata na kuheshimu taratibu zote za kimkataba na SportPesa.”

“Mazungumzo yetu yalikuwa wazi katika kusaini mkataba na Haier. Hatuwezi kuitumia SportPesa katika michuano ya CAF, hivyo Young Africans iliona inaweza kutafuta mdhamini mwingine wa muda”

“Tuna mawasiliano yote wakati tunafanya nao. Lakini si vyema kuweka wazi kila kitu. Taratibu za kiutendaji zinakwenda vyema na tutatapokuwa tumemaliza kila kitu tutakuja kukiweka hadharani “

Young Africans ilisaini Mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya SportPesa wenye thamani ya Shilingi Bilioni 12.335 mwanzoni mwa msimu huu 2022/23.

Robertinho aanika ramani ya Ubingwa
Simba SC yafafanua alipo Juma Mgunda