Uongozi wa Young Africans umeweka wazi kuwa, kweye mechi mbili zijazo za kimataifa ambazo watacheza hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, watapambana kufanya kweli ili kupata matokeo mazuri.

Young Africans ina mechi hizo dhidi ya USM Alger ambapo itaanzia nyumbani Uwanja wa Mkapa, Dar, Mei 28, 2023, kisha ugenini Juni 3, 2023 nchini Algeria.

Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema kazi kubwa iliyopo kwa sasa ni kwenye mechi za kimatafa na ambacho wanahitaji ni matokeo chanya.

“Afrika inafuatilia hasa ukizingatia kwamba fainali hii tunakwenda kuandika historia, tunahitaji kufanya kweli ukizingatia kila mchezaji na benchi la ufundi wapo tayari kwa mapambano.

“Tunachohitaji ni kupata ushindi kwenye mchezo wetu wa nyumbani, tunajua kwamba utakuwa na ushindani mkubwa, lakini kikubwa ni kupambana kupata matokeo mazuri.

“Kwa upande wa mashabiki ni muda wao kuendelea kuwa karibu na timu na kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao,” amesema Kamwe

Wanawake wenye ndoto za uongozi watakiwa kuongeza ujasiri
Opare, Sey warudisha matumaini Dodoma Jiji