Uongozi wa klabu ya Young Africans umethibitisha kuachama na meneja wa media za klabu hiyo Dismas Ten, baada ya mkataba wake kufikia kikomo.

Young Africans imethibitisha maamuzi hayo kupitia taatifa maalum iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii leo Alhamisi (Julai 29) jioni.

Klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati imemtakiwa kila la kheri Dismas Ten katika maisha yake nje ya Young Africans.

Ten alijiunga na Young Africans July 2017 kama Afisa Habari akitokea klabu ya Mbeya City na akiwa klabuni hapo amewahi kuwa Afisa Habari, Kaimu katibu mkuu, Meneja wa Timu, Afisa masoko na Sasa anaondoka akiwa Meneja wa Media za Young Africans.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 30, 2021
Gomes akabidhi ripoti Simba SC, asisitiza usajili wa kiwango