Kamati  ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Desemba 22, 2020, ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo:

Kamati hiyo imeamua kuwa, kufuatia klabu ya Singida United kushushwa madaraja mawili, mchezo wa Azam Sports Federation (ASFC) namba 65 kati ya Young Africans v Singida United uliokuwa uchezwe Jumamosi Desemba 26, 2020, hautakuwepo, hivyo Young Africans sasa wanasubiri kucheza raundi ya nne 2021.

Ilamfya apigiwa hesabu Mtibwa Sugar
Mwamuzi Elly Sasii aonywa