Orodha ya wachezaji 28 wa klabu ya Young Africans waliosajiliwa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika 2021/22, imeanikwa hadharani kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ya michuano hiyo.

Young Africans itacheza dhidi ya Rivers United ya Nigeria Jumapili (Septemba 12), Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku wapinzani wao wakiripotiwa kuwasili jijini Dar es salaam jana Jumatatu (Septemba 06).

Wachezaji wa klabu hiyo waliosajiliwa, upande wa walinda lango wapo watatu (3) ambao ni Diarra Djigui, Erick Johola na Ramadhan Kabwili huku mabeki wakiwa tisa (9) ambao ni Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Yannick Bangala, Dickson Job, Bakari Mwammnyeto.

Wengine ni Kibwana Shomari, Djuma Shaban, David Bryson, Adeyun Saleh na Paul Godfrey ‘Boxer’

Viungo wapo sita (6) ambao ni Mukoko Tonombe, Khalid Aucho, Feisal Salum Abdallah, Zawadi Mauya, Deus Kaseke, Jesus Muloko na Farid Mussa.

Washambuliaji wapo watano (5) ambao ni Fiston Mayele, Heritier Ebenezer Makambo, Yacouba Songne, Said Ntibazonkiza na Yusuf Athuman.

Hata hivyo, Young Africans itakuwa na nafasi 12 za kuongeza mastaa wengine endapo itafanikiwa kutinga hatua ya makundi ya ligi hiyo baada ya kushindwa kutumia nafasi hiyo katika usajili wa sasa.

Endapo Young Africans itafanikiwa kushinda kwenye michezo yote miwili dhidi ya Rivers United, itakutana na mshindi kati ya Fasil Kenema ya Ethiopia dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Taifa Stars kusaka alama tatu leo
Young Africans yanoa makali ya ushambuliaji