Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi Young Africans, wamelazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya KMKM leo Ijumaa (Januari 07), Uwanja wa Aman Kisiwani Unguja-Zanzibar.

Sare hiyo imeivusha Young Africans hadi hatua ya nusu fainali kwa kufikisha alama 4, hivyo magwiji hao wanaendelea kutetea vyema taji lao.

Hata hivyo Young Africans imefuzu hatua ya nusu fainali kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Mabao ya Young Africans yaliwekwa nyavuni na Heritie Makambo na bao lingine likifungwa na Feisal Salumu ambaye ndiye nyota wa mchezo huo.

Ufunguo wa Gereza la Mandela, Tunu Afrika Kusini
Vita ya wenyewe Ethiopia, Maafa yahamia kwa watoto