Kocha wa klabu ya Young Africans Cedric Kaze amesema kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi itakayoanza kesho (Januari 05) kisiwani Unguja atawatumia wachezaji ambao huwa hawapati nafasi kwenye kikosi chake cha kwanza.

Young Africans wanatajia kuondoka jijini Dar es salaam leo Jumatatu (Januari 04) kuelekea kisiwani Zanzibar tayari kwa michuano hiyo, ambayo hufanyika kila mwaka, kwa ajili ya kusherehesha maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo kilele chake ni Januari 12.

Kaze amesema anaamini wachezaji watakaopata nafasi ya kushiriki kwenye michuano hiyo, watafanya vizuri na kufikia lengo la kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.

Hata hivyo kocha huyo amesema wachezaji sita walioitwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars),kwa ajili ya michuano ya Mataifa Bingwa Barani Afrika (CHAN), hawatokua sehemu ya safari ya kuelekea Unguja – Zanzibar.

Kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2021 Young Africans imepangwa Kundi A lenye timu za Jamuhuri na Namungo FC.

Kundi B: Simba SC, Mtibwa sugar na Chipukizi fc

Kundi C: Azam FC, Malindi FC na Mlandege fc

Young Africans wataanza kampeni ya kusaka ubingwa wa Kombe la Mapinduzi mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Jamhuri FC kesho Jumanne (Januari 05).

Mchezo mwingine utakaochezwa kesho Jumanne utakua kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Chipukizi.

06, 01, 2021

Malindi FC  v  Mlandege

07, 01, 2021

Simba SC  Chipukizi

08, 01, 2021

Azam FC v  Mlandege FC

Young Africans  v  Namungo FC

09, 01, 2021

Jamhuri  FC  v  Namungo FC

Simba sc  v  Mtibwa sugar

10, 01, 2021

Azam FC  v  Malindi FC

Maalim Seif : Hakutakuwa na ubaguzi Zanzibar
Maguri: Tumekuja kupambana