Baada ya kukanusha kilichosemwa na wengi, hatimaye rapper Young Dee ametoka hadharani na kukiri kutumia dawa za kulevya na kuwaomba radhi mashabiki na jamii kwa ujumla.

Rapper huyo ambaye aliwahi hata kukanusha kupitia wimbo wake wa ‘Tetesi’ amesema kuwa ametumia dawa hizo kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na kwamba hivi sasa ameachana nazo na kuahidi kutoyagusa tena.

Akiongea na wadau wa muziki leo katika ukumbi wa Escape One jijini Dar es Salaam, Young Dee ameeleza kuwa amerejea rasmi kwenye uongozi wake wa zamani wa Million Dollar Boyz, MDB alioachana nao mwaka jana.

Hivi karibuni, Young Dee na meneja wake wa zamani Max Rioba walianza kupost picha zilizoashiria kumaliza tofauti zao.

 

Makonda Feki Akamatwa Dar
Kitila Mkumbo: Tuna tatizo katika pande zote za siasa