Rapa Young Killer Msodoki toka Mwanza, kwa mara ya kwanza amefungua milango ya fursa za ajira kupitia kipaji chake kwa yeyote mwenye uwezo wa kuandika mashairi.

Young Killer ambaye hajawahi kuandikiwa mashairi, amesema kuwa yeyote ambaye anaamini kuwa anaweza kuandika mashairi yenye uzito unaofanana na rapa huyo, ajitokeze na atampa nafasi hiyo.

“Nishaonyesha uwezo mkubwa na sikuwahi kuandikiwa nyimbo hata siku moja toka nimeanza. Sasa nafungua dirisha la usajili kwa yeyote anayetaka kuniandikia ngoma kali iwe na uwezo ambao ni mkubwa kama mimi au zaidi,” Young Killer aliuambia mtandao wa Bongo5.

Rapa huyo ambaye hivi karibuni ameachia wimbo wa ‘Mtafutaji’ alioufanya kwa swag tofauti, pia amewakaribisha watayarishaji wachanga nchini kumuandalia kazi zake.

 

Video: Makonda awataka wafanyabiashara kuwa wastaarabu
Paul Pogba: Nipo Tayari Kuwakabili Southampton