Klabu ya Yanga imetangaza ajenda kumi na moja kwa ajili ya mkutano mkuu wa dharura uliopangwa kufanyika Oktoba 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaunda jijini Dar es Salaam.

Katika ajenda hizo, moja imeeleza kuwa katika hotuba yake, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, atawataja maadui wa klabu hiyo, huku kukiwa na msisitizo kuna mamluki wa wafanyabiashara wanaofanya mbinu za kuivuruga Yanga.

Pamoja na ajenda nyingine 10, hiyo moja inaonekana kuanza kuwa gumzo kwenye mitandao, hasa kuhusiana na kwamba Manji atawataja maadui hao wa Yanga, ikielezwa wamepania kushusha hadhi ya klabu hiyo ili kuonyesha Manji ameshindwa.

“Kutakuwa na hotuba ya mwenyekiti, maoni na msimamo wake juu ya maazimio ya wanachama na kusema anayoyajua ya siri kuhusu Yanga na adui wa Yanga.

“Pia atafafanua wanaoleta vurugu, baadhi ni mamluki wa wafanyabiashara wenzake walioshindwa kumshinda kwa njia halali na sasa wanaitumia Yanga kama sehemu pekee iliyobaki kumuumiza kupitia mbinu zinazotumika.

“Mbinu hizo ni kuleta vurugu ndani ya Yanga ili kumchafua binafsi ili kushusha hadhi ya klabu,” ilieleza sehemu ya ajenda hiyo ya kumi na moja.

Ajenda nyingine zilizotajwa ni pamoja na kupitia dondoo za kikao kilichopita, kuthibitisha wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, suala la kukodisha timu na nembo, kumjadili mwenyekiti (Manji) kuhusiana na kampuni inayotaka kukodisha ambayo ni yake na kubaki kwake katika uenyekiti.

Itakuwa ni mgongano wa mawazo, kupitia utendaji wa kamati ya mashindano, kujadiliwa kwa wanachama ambao hawafiki kwenye vikao na wanakosoa kwenye vyombo vya habari tu na kujadili tarehe ya uchaguzi mdogo kujazia nafasi za wajumbe wa kamati ya utendaji.

Yanga iliamua kuitisha mkutano huo wa dharura baada ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza halitambui klabu hiyo kuikodisha timu yake na nembo yake kwa Kampuni ya Yanga Yetu Ltd.

Mkutano huo unasubiriwa kwa hamu, kwani hivi karibuni Manji alionekana kuudhika na kuendelea kusakamwa hadi kufikia kuona ajitoe Yanga. Lakini mwisho akabadili uamuzi na kusema, mkutano huo wa wanachama ndiyo utaamua juu yake kwa kuwa wanachama wengi wamekuwa wakimuunga mkono.

AJENDA ZA MKUTANO MKUU WA DHARURA WA WANACHAMA TAREHE 23 OKTOBA, 2016 KWENYE UWANJA WA KAUNDA.

 1. SALA NA UTAMBULISHO WA WAGENI WAALIKWA:

1.1.    Sala ya Wakristo ya Kubariki Kikao.

1.2.    Sala ya Waislamu ya Kubariki Kikao.

1.3.    Utambulisho wa wageni waalikwa waliohudhuria, pia wenye udhuru – Waziri wa Michezo na Sanaa; Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT), Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Dar-Es-Salaam (DRFA) na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 2.       KUFUNGUA KIKAO.

 1. KUPITIA DONDOO ZA KIKAO KILICHOPITA CHA MKUTANO WA WANACHAMA NA KUIDHINISHA.
 2. KUTHIBITISHA WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI NA KUMPUMZISHA MJUMBE MMOJA NA KUONGEZAMJUMBE MWINGINEKWENYE BARAZA LA WADHAMINI.

MWENYEKITI KUOMBA RIDHAA YA KUMTEUA MJUMBE MMOJA BILA YA KUITISHA MKUTANO MKUU KUPUNGUZA GHARAMA KWAKLABU.

 1. KUPITIA NA KUJADILL MUHTASARI YA MAKUBALIANO YA BODI YA WADHAMINI KULINGANA NA MAAGIZO YA WANACHAMA KUKODISHA TIMU YA YANGA NA NEMBO YA YANGA KWA KIPINDI CHA MIAKA KUMI/ NA KUPATA MAAMUZI KUPITIA KURA ZA WANACHAMA.
 2. KUJADILI MWEYEKITI ABAKI KAMA MWENYEKITI AU KULINGANA NA MASLAHI YAKE KWENYE KAMPUNI, KAMA ITALETA MGONGANO KATIKAMPUNI YAKE INAYOKODISHA TIMU YA YANGA NA NEMBO YA YANGA KWA KIPINDI CHA MIAKA KUMI ILI KUPATA MAAMUZI KUPITIA KURA ZA WANACHAMA.
 3. KURUDIA KUPITIA MAREKEBISHO YA KATIBA ILIYOAGIZWA NA WANACHAMA KUPITIA VIKAO VYAO MBALIMBALI NA BAADHI KUKATALIWA NATFF, BAADHI HAZIJASAJILIWA KAZI NA BMT NA BAADHI RITA WAMEZIKALIA BILA KUZIFANYIA KAZI KWA SABABU ZISIZOJULIKANA. KUPATA MSIMAMO WA WANACHAMA KWA KUZINGATIA KATIBA YA YANGA INAYOSEMA MIKUTANO YA WANACHAMA NDIO YENYE MAMLAKA YA MWISHO ILIMRADI TU MAAMUZI HAYO YAANGUKIE NDANI YA SHERIA ZA NCHI NA SI SAHIHI VYOMBO HIVYO KUINGILIAA MAAMUZI HALALI YA WANACHAMA.
 4. KUPITIA UTENDAJI WA KAMATI YA MASHINDANO, RATIBA YA LIGI KUU BARA, ADHABU YA YANGA KUTOKA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO AMBAYO ILISABABISHWA NA FUJO ZA MASHABIKI WA SIMBA.
 5. KUPATA MAAMUZI JUU YA WANACHAMA AMBAO HAWAFIKI KATIKA MIKUTANO BADALA YAKE WANAKUWA WASEMAJI WA YANGA BILA KUWA NA MAMLAKA HAYO NA KULETA UCHONGANISHI WA WAZI NDANI YA KLABU, KUPOTSOHA JAMII NAKUCHAFUA MAJINA YA VIONGOZI WA KLABU.
 6. TAREHE YA UCHAGUZI MDOGO KUJAZIA NAFASI ZILIZO WAZI NA KUPATA MWONGOZOWAKUTUMIA KATIBA IPI KATI YA 2010 AU 2014.PAMOJANA MASAHIHISHO BAADA YA 2014, AU BILA YA MASAHIHISHO YA 2014 YALIYOAMULIWA NA WANACHAMA.
 7. HOTUBA YA MWENYEKITI –MAONI NA MSIMAMO WAKE JUU YA MAAZIMIO YA WANACHAMAKWENYE KIKAO;

KUSEMA ANAYOYAJUA YA SIRI KUHUSU YANGA NA ADUI WA YANGA NA KUFAFANUA WANAOLETA VURUGU YANGA, BAADHI NI MAMLUKI WA WAFANYABIASHARA WENZAKE WALIOSHINDWA KUMSHINDA KWA NJIA HALALI NA SASA WANAITUMIA YANGA KAMA SEHEMU PEKEE ILIYOBAKI KUMUUMIZA KUPITIA MBINU ZINAZOTUMIKA HASA KWA KULETA VURUGU NDANI YA YANGA ILI KUMCHAFUA YEYE BINAFSI, KUFANYA KWAO HIVYO NI KUSHUSHA HADHI YA KLABU NA MAONI YAKE KWA MASLAHI YA YANGA, KIPI KIFANYIKE.

 1. MENGINEYO.
 2. SALA.

13.1.  Sala ya Waislamu ya Kubariki Maamuzi ya Mkutano.

13.2.  Sala ya Wakristo Kubariki Maamuzi ya Mkutano.

 1. KUFUNGA MKUTANO.
ATCL Yatoa Ofa ya Mwezi Mmoja
Pluijm Ataja Sababu Za Kumuweka Benchi Ali Mustapha ‘Barthez’