Klabu ya Kagera Sugar huenda ikamrudisha kikosini Kiungo Mshambuliaji Yusuph Mhilu kutoka Simba SC, kufuatia mchezaji huyo kuwa kwenye mpango wa kuuzwa kwa mkopo, katika kipindi hiki cha Usajili wa kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa, inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Singida Bog Stars FC ambayo itashiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2022/23, nayo inatajwa kuwa kwenye mpango wa kumsajili kwa mkopo Kiungo huyo, ambaye ameshindwa kuonyesha uwezo wake akiwa Simba SC msimu wa 2021/22.

Kagera Sugar ipo kwenye mchakato wa kuingia kwenye dili la kumuwani Mhilu, baada ya kuachana na Hassan Mwatelema anayedaiwa kushindwana na Uongozi wa klabu hiyo, upande wa maslahi kupitia mkataba mpya aliotakiwa kuusaini siku kadhaa zilizopita.

Mwatelema anatajwa kuwa kwenye mpango wa kusajiliwa Dodoma Jiji FC ambayo imeonyesha nia ya kuhitaji huduma yake kwa msimu ujao.

Kagera Sugar inapewa nafasi kubwa ya kumnasa Mhilu tofauti na Singida Big Stars, kufuatia ukaribu uliopo kati ya mchezaji huyo na viongozi wa wababe hao wa Kaitaba Stadium.

Hadi sasa Uongozi wa Simba SC haijasema lolote kuhusu kuondoka kwa Mhilu katika kipindi hiki, lakini inatajwa wakati wowote kuanzia sasa huenda wakaliweka wazi suala hilo.

Mhilu alijiunga Simba Sc mwanzoni mwa msimu wa 2021/22, baada ya kumaliza mkataba wake na Kagera Sugar FC.

Kega ‘amuwashia moto’ Gachagua
Ahmed Ally atoka na jipya usajili Simba SC