Mchezaji wa Crystal Palace, Wilfried Zaha ameachana na wakala wake kwa kushindwa kufanikisha mpango wake wa kuihama klabu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu huu mpya wa ligi kuu soka ya nchini uingreza.

Zaha ambaye pia ni winga wa timu ya taifa ya Ivory Coast  alikuwa anahitaji kuachana na Palace kabla ya msimu huu kuanza ambapo baadhi ya vilabu nchini humo vimekuwa vikimuhitaji ikiwemo Everton na Arsenal lakini Will Salthouse ambaye ni wakala wake huyo amedaiwa kutofanya kazi yake ipasavyo na kusababisha mchezaji huyo kusitisha kuendelea kufanya kazi nae.

Mchakato wa Zaha kuihama timu hiyo ulishindikana  baada ya klabu yake kuweka dau la pauni milioni 80 ambayo ni sawa na bilioni 226 za Tanzania kwa klabu yoyote ambayo ingehitaji huduma ya mchezaji huyo jambo ambalo limeonekana kuwa gumu.

Taarrifa zinasema  kuwa Zaha alimwambia Salthouse kuhusu maamuzi yake ya kuondoka kwenye klabu hiyo yake lakini ikashindikana na ndipo mpango ukashindikana na akafikia maamuzi ya kutoendelea kufanya kazi na wakala wake huyo.

Washtakiwa wa kigeni wakwamisha kesi ya “MO”
Neymar kujisafisha Paris Saint-Germain