Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema leo Jumatatu anatarajia kukutana na uongozi wa timu hiyo lengo likiwa ni kudai stahiki zake, alipwe kwa wakati.

Zahera ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kuwasili chini akitokea DRC akiahidi ataidai klabu hiyo aliyokuwa akiinoa hapo awali.

Zahera alisema baada ya kutua nchini alionana na baadhi ya viongozi waandamizi wa timu hiyo na kukubaliana kuwa wakutane Jumatatu katika makao makuu ya klabu hiyo.

“Nikweli nimefika na nimeonana na baadhi ya viongozi, lakini wameniahidi tutakutana wiki ya Jumatatu kwa kuwa kwa sasa viongozi wengi wamesafiri na timu kwenda mkoani Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu, “alisema Zahera .

Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kama uongozi wamekubali kulipa stahiki zake zote kwa kocha huyo na kwamba kama walikuwa tayari kuachana naye basi wameshajipanga kumlipa.

“Kikubwa kwa sasa tunasubiri tukutanane naye tufanye majumuisho tumlipe chake kwa sababu sio ugovi na wala sio shari tunajua alitufanyia kazi tutamlipa wala hakuna mashaka yoyote,” alisema Mwakalebela.

Zahera alifungashiwa virago na uongozi wa timu hiyo mwezi uliopita kufuatia timu hiyo kushindwa kupata matokeo chanya katika mechi za Ligi Kuu na kutolewa kwenye michuano ya kimataifa na nafasi yake kuchukuliwa na Charles Mkwasa.

Kipande cha ubao wa zizi la Yesu charejeshwa Bethlehem
Utata waibuka kifo cha kichanga baada ya kufanyiwa Tohara