Mkurugenzi wa ufundi wa Gwambina FC Mwinyi Zahera amesema huenda mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC wakapata matokeo dhidi ya AS Vita Club, kwenye mchezo wa kwanza wa ‘Kundi A’ wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba SC watacheza mchezo huo kesho Ijumaa (Februari 12) mjini Kinshasa, huku ikkubukwa waliwahi kupoteza dhidi ya AS Vita kwa kufungwa mabao matano kwa sifuri msimu wa 2018/19, kabla ya kuibuka na ushindi wa mabo mawili kwa moja jijini Dar es salaam.

Zahera ambaye aliwahi kuwa kocha mku wa Young Africans amesema katika mchezo wa kesho Ijumaa anawapa Simba SC 60% , huku wenyeji AS Vita Club akiwapa 40%.

Kocha huyo kutoka DR Congo ametoa sababu ya kutoa asilimia hizo kwa timu hizo kwa kusema Simba msimu huu ina kikosi kizuri na imefanya maandalizi ya kutosha, tofauti na ilivyokua msimu wa 2018/19, huku akiamini AS Vita Club wana udhaifu mkubwa katika kipindi hiki.

“AS Vita Club iliyoifunga Simba mabao matano kwa sifuri imesambalatika kwa kuwa wachezaji karibu kumi  waliokuwepo kikosini wameondoka wakiwemo Fabrice Ngoma, Jean Makusu, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda na wengine”

“Kwa jinsi nilivyoiona AS Vita katika mechi 5 za ligi hapa Congo DR, nawapa Simba asilimia 60 ya kushinda na AS Vita nawapa asilimia 40 ya kushinda mchezo huu kwa sababu ina vijana wengi ambao hawana uzoefu”

“Kwa jinsi ninvyoiona Simba ya msimu huu na AS Vita ya msimu huu, naona Simba imekamilika kwa maana ya mbele wako vizuri, katikati wako vizuri na nyuma wako vizuri pia.” Amesema  Mwinyi Zahera.

Simba SC tayari imeshawasili mjini Kinshasa, Dr Congo na jana usiku iliendelea na mazoezi ikiwa mjini humo, tayari kwa mchezo dhidi ya AS Vita Club utakaoanza mishale ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Mbunge avunja ukimya tatizo la kupumua linavyoua watu
Mwamnyeto safi, Ntibazonkiza atuma ujumbe