Jumla ya Wanaume 520, wameripotiwa kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo kudhalilishwa kwa kipigo na kunyimwa unyumba na wenzi wao baada ya kukosa ajira, katika kipindi cha mwezi Januari – Septemba, 2022 nchini Zambia.

Kufichuka kwa matukio hayo kunafuatia uwepo wa kesi za unyanyasaji wa kijinsia ambazo zilisababisha kufanyika kwa utafiti sehemu mbalimbali za nchi kupitia Shirika lisilo la kiserikali la Mtandao wa Kitaifa wa Wanaume wa Jinsia na Maendeleo ya Zambia, (ZNMNGD).

Shirika hilo lisilo la faida, la kukuza usawa wa kijinsia na maendeleo kupitia ushiriki wa wanaume na wavulana kama washirika katika kutoa changamoto kwa aina zote za ukosefu wa usawa wa kijinsia, linasema suala la ukosefu wa ajira kwa wanaume limekuwa ni fimbo ya kuwachapia Wanaume.

Mfano wa matukio yanayodaiwa kuripotiwa kwa Wanaume kupigwa na wenzi wao. Picha na The chronical.

Mratibu wa kitaifa wa ZNMNGD, Nelson Banda anaamini kuwa kesi hizo 520 zilizorekodiwa, ni dhibitisho kwamba kuna wanaume zaidi ambao wananyanyaswa na wenzi wao na wengi wamekuwa kimya kutokana na kuona aibu ya kulizungumzia suala hilo.

Banda anasema, “Waathiriwa wengi walilalamika kudhulumiwa kimwili, kingono na kihisia na wapenzi wao na wanasema wamekuwa wakiona aibu kusimulia mambo hayo lakini majeraha yatokanayo na vipigo yamekuwa yakifichua siri na hivyo kuomba msaada.

Hata hivyvo, watetezi wa haki za binadamu wamepigia kelele suala hilo, na kusema halina mashiko kwani kukosa ajira hakutokani na uzembe isipokuwa ni hali ya mataifa mengi ya kukumbwa na mtikisiko wa kiuchumi uliosababishwa na mambo kdhaa ikiwemo maradhi ya Uviko-19, vita nchini Ukraine na mabadiliko ya tabianchi.

Ofisi ubalozi wa Ufaransa zavamiwa, zachomwa moto
Twende na kasi ya Rais utengaji maeneo uwekezaji: Dkt. Mabula