Mapigano kati ya jeshi la Libya na wapiganaji wa Islamic State yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 30.

Msemaji wa hospitali moja alisema kuwa wapiganaji 36 wameuawa huku wengine karibu 140 wakijeruhiwa katika mji wa Sirte ambao ni ngome ya Islamic state.

Wakati huo huo taarifa zinasema kuwa idadi ya watu waliouawa wakati mlipuko ulitokea katika ghala la silaha kwenye mji ulio magharibi wa Garabulli imeongezeka hadi watu 29.

Ghala hilo liliripotiwa kuwa ndani ya kambi inayotumiwa na wapiganaji kwenye mji wa Misrata pwani ya nchi.

Serikali Yapokea Msaada Wa Madawati 300 Kutoka Ubalozi Wa Kuwait
Makonda Feki Akamatwa Dar