Rais Samia Suluhu Hassan amesema tangu kupokelewa kwa chanjo ya UVIKO-19 mwezi Julai na kuzinduliwa Rasmi jijini Dar es salaam tar 28 Julai zaidi ya watu 800,000 wameshapata chanjo hiyo ya kujikinga na maambukizi ya UVIKO-19.

Rais Samia amesema hayo leo katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19 ambao alikua Mgeni Rasmi.

Samia amewaasa wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kwa kuwa kujikinga na Gonjwa hilo kutaendelea kukuza uchumi wa nchi na maslahi binafsi na kuongeza kuwa watu wa rika mbalimbali wamekua wakijitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo na kwa nyakati tofauti pamoja na sintofahamu iliyotokea hapo mwanzo juu ya uhalali na Ukweli wa chanjo hiyo

Rais Samia ameishukuru Shirika la Fedha Duniani IMF kwa kutoa mkopo nafuu wa Sh. trilion 1.3 ikiwa Mpango huu wa kuinua Uchumi na Kukabiliana na UVIKO-19 wa Mwaka mmoja una Jumla ya thamani ya Shilingi Trilioni 3.62.

Wadau wengine wa maendeleo ambao Serikali ipo katika mazungumzo nao ili kuunga mkono Juhudi hizi za kuinua Uchumi ni Benki ya Dunia na Umoja wa Ulaya.

Katika hatua nyingine Rais Samia Suluhu Hassan amesema Ukuaji wa pato la Taifa kwenye Robo ya pili ya Mwaka 2021, Uchumi umeongezeka hadi kufikia 4.3% ukilinganisha na 4% kipindi ka hicho mwaka uliopita ikiwa pia Nchi imeweza kudhibiti Mfumuko wa Bei ambao umeendelea kuwa na tarakimu 1.

“Tumeweza Kulipa Madeni ya nje na ya Ndani ya Nchi yetu, tumemaliza uhakiki wa madeni ya ndani yanayotokana na madai ya watumishi, wazabuni, wakandarasi, madeni ya Huduma za umeme na maji, na simu kwa taasisi za umma na madeni ya Fidia na malipo ya bima za ajali” amesema Rais Samia.

Sitaki utitiri wa Kamati:Rais Samia
Wananchi wa Bukombe wagawiwa Kondomu usiku wa mkesha wa Mwenge