Siku ya wakimbizi duniani tarehe 20 juni, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameyahimiza mataifa yaliyoendelea duniani kutoa fursa zaidi kwa wakimbizi wanaosaka makazi mapya.

Gutteres amesema kutokana na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linalosema kutokuwa na uhakika wa chakula duniani kote, janga la mabadiliko ya tabianchi, vita nchini Ukraine na dharura nyinginezo kuanzia Afrika hadi Afghanistan ndio sababu kubwa zilizowafanya watu milioni 100 kufungasha virago na kukimbia makwao.

Gutteres ameyasema hayo alipowatembelea wakimbizi kutoka nchini Iraq na Afghanistan wanaoishi jijini New York Marekani. 

“Kama mamilioni ya wakimbizi duniani kote, wanasaidia kuleta maisha mapya, ustawi na utofauti tajiri kwa jumuiya zinazowapokea. Ni lazima tuendelee kuwaunga mkono,” mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema kwenye akaunti yake ya Twitter kufuatia ziara hiyo.

Guterres, ambaye alikuwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kuhudumia wakimbizi kuanzia mwaka 2005 hadi 2015, amesisitiza nafasi muhimu ya mataifa yaliyoendelea katika kupokea wakimbizi na kuwapa fursa, yeyote yule na popote anapotoka.

Katika taarifa za UNHCR, vita ya Ukraine imesababisha janga kubwa zaidi la uhamishaji wa watu ulimwenguni kwa kuwa mamilioni ya wakimbizi wamevuka na kuingia katika nchi jirani, na wengi zaidi wamekimbia makazi yao ndani ya nchi.

Shirika hilo linasema kutokuwa na uhakika wa chakula duniani kote, janga la mabadiliko ya tabianchi, vita nchini Ukraine na dharura nyinginezo kuanzia Afrika hadi Afghanistan ndio sababu kubwa zilizowafanya watu milioni 100 kufungasha virago na kukimbia makwao.

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limeanza tena oparesheni zake za hiyari kuokoa maisha kwa kusafirisha wahamiaji VHR kutoka Yemen hadi Ethiopia mwezi huu na linalenga kuwasaidia wahamiaji wasiopungua 6,750 wanaotoka Ethiopia kuondoka katika nchi hiyo iliyoathiriwa na migogoro.

Kwa upande mwingine UNHCR ina hofu kubwa juu ya ongezeko la mashambulizi na ghasia vinavyofanywa na makundi yalioyjihami dhidi ya raia nchini Burkina Faso.

Ingawa idadi ya wakimbizi na wahamiaji wanaovuka bahari ya Mediteranea kwenda Ulaya imepungua, idadi ya wanaokufa imeongezeka, kwa kuwa safari ni za hatari zaidi, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Kwa mujibu wa UNHCR, Waafghan ni miongoni mwa idadi kubwa ya wakimbizi duniani kote. Kuna wakimbizi milioni 2.6 waliosajiliwa kutoka Afghanistan kote ulimwenguni, kati yao milioni 2.2 wamesajiliwa nchini Iran na Pakistan pekee.

Umoja wa Mataifa unasema dunia ilifikia hatua ya kushangaza ya wakimbizi milioni 100 mwezi Mei, 2022, wiki 10 baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kuwafukuza sio tu watu waliokimbia vita lakini pia ulisababisha ukosefu wa chakula duniani, pamoja na uhaba wa nafaka na mbolea.

Serikali yaainisha maeneo ya hifadhi na vijiji
Malota Soma: Uchovu umeigharimu Simba SC