Watumsihi wa Umma 14,409 wamebainika kuwa na vyeti feki huku watumishi 1,907 bado hawajawasilisha vyeti vyao kuhakikiwa licha ya Serikali kutoa muda wa kutosha kuwasilisha vyeti vyao Baraza la Mtihani la Tanzania (NECTA) kwa uhakiki, na watumishi wengine 71 wamebainika kuwa na majina tofauti yaliyoandikishwa kwenye orodha ya majina ya waajiriwa na yale yaliyopo kwenye vyeti vyao.

Taarifa hiyo imetolewa jijini Dodoma na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA), Dk. Charles Msonde wakati akiwasilisha taarifa ya sita ya mwisho ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma vya ufaulu wa kidato cha nne, cha sita na ualimu kwa katibu Mkuu – Utumishi Dk, Lauren Ndumbaro.

Msonde amesema katika awamu ya sita, watumishi 5,696 wamehakiki vyeti vyao kati ya hao 5404 sawa na 94% wamebainika kuwa na vyeti halali na watumishi 294 sawa na 5% wamebainika kughushi vyeti.

Kufuatia hata hiyo Ndumbaro amesema majina ya watu ambao taarifa zao katika awamu ya tano zimebainika kuwa ni feki anaamini kuwa wameshaondolewa katika orodha ya malipo kama wafanyakazi wa umma.

Pia ameagiza hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya watumishi 1,907 ambao mpaka sasa wamekaidi agizo la Rais Magufuli la kuwasilisha vyeti vyao kwa ajili ya uhakiki, na kuwataka wote waliobainika kuwa na vyeti feki kama hawajiridhishwa na matokeo ya uhakiki wamepewa fursa ya kukata rufaa hadi tarehe 31 machi mwaka huu.

 

Jerry Muro: Tusiruhusu ushabiki uondoe uzalendo wetu, Hongera Swahiba
Mshauri wa Trump ajing'atua nafasi yake