Mkuu wa Wilaya Pangani, Zainab Abdalah, ambaye siku zilizopita alitoa kali ya mwaka iliyotikisa hisia za watu wengi na kuibua mijadala mtandaoni baada ya kumuomba mume wake aoe mke mwingine akidai kuwa majukumu yamekuwa mengi hivyo anahitaji msaada wa kumlea mume.

Leo katika ukurasa wake wa instagram ametoa ujumbe mzito kwa jamii akijaribu kukumbusha kuwa leo ni siku ya ibada kwa waislamu hivyo ni vyema kulea nafsi zetu katika misingi mizuri ya ibada na kumcha Mungu kwani, siku ya kifo mali, ndugu, jamaa, marafiki, familia, nafasi tulizonazo katika jamii, vyote ni vitu vya kupita, na siku hiyo tutaambatana na nafsi zetu, hivyo tukiwa duniani ni vyema kutenda matendo ya ibada.

Kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika ujumbe huu mrefu ulioambata na stori nzuri yenye mafunzo makubwa ndani yake.

”Kulikuwa na Mzee ana wake wanne, ghafla akaumwa sana na aliona kabisa umauti unamkaribia. Akaamua kuzungumza na wake zake kila mmoja akiwa peke yake. Akaanza kumuita Mke wa nne, akamuuliza; mimi nakaribia kufa, je utaenda na mimi kaburini? Mke akajibu Hapana kwa kweli sitaweza, utaenda peke yako. Akamuuliza Mke wa tatu; je utaenda na mimi kaburini? Akajibu, hapana sitaweza tena ukizikwa tu naolewa na mume mwengine. Akamuuliza Mke wa pili; je utaenda na mimi kaburini? Akamwambia; hapana sitaweza ila nitasimamia mazishi yako mpaka mwisho, huo ndo utakuwa mchango wangu. Akamuuliza Mke wa kwanza; je utaenda na mimi kaburini? Akajibu; Naam nitaenda na wewe kaburini, tutazikwa wote na nitasimama na wewe mpaka siku ya hukumu.

Moral of the story: Fundisho la stori hii.
Mke wa nne ni mali na fedha, vitu ambavyo tukiwa duniani tunavipenda sana na kuona ndo vina maana kuliko kitu chochote. Lakini tukifa vinatuacha tunaenda wenyewe kaburini. Mke wa tatu ni vyeo au status, ambapo ukiondoka vinahamia kwa mtu mwengine na unaenda kuzikwa mwenyewe. Mke wa pili ni ndugu na marafiki wa karibu, ambao ukiondoka watasimamia taratibu zote za mazishi, watalia ila hawataweza kwenda kuzikwa na wewe. Na Mke wa kwanza ni nafsi, ni kitu ambacho tunakipuuza na kukidharau kumbe ndo kitu pekee ambacho tutaondoka nacho duniani.

M/Mungu atujaalie tuwe wenye kuzilea nafsi zetu ziwe zenye kumcha Mungu na kuwa na khofu na Mungu. Atupe nafsi za kutenda mema na kujiepusha na mabaya. Ziwe nafsi za kutuondoa na adhabu za duniani na kesho akhera. Ameen?. Ameandika Zainab

Amemalizia kwa kuandika ”JUMAA KAREEM?”.

Ligi kuu kuendelea leo
Rais Magufuli kuzindua ukuta machimbo ya madini leo