Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliono ya Azam FC Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amemaliza utata wa adhabu ya Penati iliyotolewa na Mwamuzi wa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi Jana (Alhamis Januari 13) uliowakutanisha dhidi ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC.

Mlinda Lango wa Azam FC Mathias Kigonya alimchezea ndivyo sivyo kiungo Mshambuliaji wa Simba SC Pappe Ousman Sakho na kusababisha tuta, ambalo liliipa bao la ushindi Simba SC.

Zakazakazi amesema Tuta lililotolewa na Mwamuzi kufuatia kosa la Mlinda Lango wao Kigonya, liliku halali na haoni sababu ya wadau wa soka nchini kuendelea kupiga kelele kwa madai Simba SC wamebebwa.

Zakazakazi amesema: “Ilikua Penati halali kabisa na Mlinda Lango wetu alipaswa kuoneshwa kazi nyekundu, lakini imekua bahati kwake kuoneshwa kadi ya njano.”

Bao la Ushindi la Simba SC lilikwamishwa kimiani na Mshambuliaji kutoka nchini Rwanda Meddie Kagere dakika ya 56.

Mwijaku akitaka Kiti cha Ndugai
Stamico:Taka ngumu ni fursa kiuchumi