Chama cha Soka nchini Zambia ‘FAZ’ kimeliomba Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ kuandaa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya Umri wa miaka 17 kwa mwaka huu.

‘FAZ’ wamewasilisha maombi hayo ‘CAF’ kwa njia ya barua na wanaamini siku kadhaa zijazo watapata majibu ambayo yatawapa uhakika wa kuwa mwenyeji wa Fainali hizo ama kukataliwa.

Zambia imeamua kujitosa kuomba nafasi ya kuwa mwenyeji mbadala wa Fainali hizo, baada ya ‘CAF’ kuzifuta Fainali hizo zilizotarajiwa kuchezwa nchini Morocco kuanzia Machi 13.

‘CAF’ walifikia maamuzi hayo mwanzoni mwa juma hili kufuatia Serikali ya Morocco kuweka vikwazo kwa Mataifa kadhaa ya Afrika kuingia nchini humo, kwa kuhofia maambukizi mapya ya virusi vya Corona.

Zambia kupitia ‘FAZ’ wamewahakikishia ‘CAF’ kuwa na uzoefu wa kutosha kuandaa Fainali hizo za vijana, baada ya kuwa wenyeji wa Fainali za vijana chini ya Miaka 20 mwaka 2017 na Fainali za Ukanda wa Afrika Kusini ‘COSAFA U20’ zilizofanyika mwaka 2019.

Tayari timu za taifa ya Zambia, Tanzania, Uganda na Ivory Coast zilikiwa zimewasili nchini Morocco kwa ajili ya ushiriki wa Fainali za vijana chini ya umri wa miaka 17 mwaka huu 2021.

No photo description available.

Serikali kuanzisha vituo vya uhakiki wa bidhaa
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera afariki