Hali ya taharuki imezuka visiwani Zanzibar baada ya watu wasiojulikana kulipua mabomu yaliyovunja nyumba kadhaa ikiwemo nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi visiwani humo, Hamdani Makame.

Kamishna Makame

Akizungumzia tukio hilo mbele ya waandishi wa habari, Kamishna Hamdani Makame ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 5 usiku.

Alisema kuwa mlipuko huo uliharibu sehemu ya paa ya nyumba na limesababisha watu kadhaa waliokuwa wamelala ndani ya nyumba hiyo kujeruhiwa pamoja na hasara iliyotokana na uharibifu wa vitu vilivyokuwa ndani ya nyumba hiyo.

Kamishna Makame amelifananisha tukio hilo na lile lililotokea Machi 3 mwaka huu katika Maskani ya Chama Cha Mapinduzi, Kisonge Mjini Unguja na kuahidi kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika.

 

Ingawa haijafahamika chanzo cha tukio hilo, inaaminika kuwa lina uhusiano na mgogoro wa kisiasa uliozua taharuki visiwani humo, ikiwa zimebaki siku 5 kabla ya kufanyika uchaguzi wa marudio uliotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha lakini unapingwa na viongozi pamoja na wafuasi wa Chama Cha Wananchi (CUF).

 

Mahakama ya Mafisadi yaiva, Waziri aiweka wazi
Magufuli: Vijana wasiofanya kazi walazimishwe, wapelekwe kambini