Daktari Massoud Abdallah, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Chake chake, pemba akikabiliwa na mashtaka ya kuomba rushwa ya ngono mgonjwa.

Daktari huyo anatuhumiwa kuomba rushwa ya ngono kwa mgonjwa ambaye ni mama mjamzito aliyefika Hospitali ya Chake chake kwaajili ya matibabu.

Mwendesha mashtaka kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka Pemba, Ramadhan Suleiman, amedai mtuhumiwa huyo alitenda makosa mawili, la kwanza likiwa la Novemba 21, mwaka huu katika hospitali ya Chake chake aliomba rushwa ya ngono kwa mgonjwa aliyekwenda hospitalini hapo kwaajili ya huduma ya uchunguzi wa Ultra Sound.

Alidai kitendo hicho ni kosa kisheria kwa kuwa ni kinyume cha kifungu cha 58 cha sheria ya rushwa namba 1 ya mwaka 2019 ya sheria za Zanzibar.

Mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo na kuiomba Mahakama impatie dhamana , ombi ambalo lilikubaliwa kwa bondi ya sh. milioni mbili.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena mwakani Febuari 27.

Awali mnamo Novemba 21 mwaka huu, Mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar (Zaeca) kisiwani Pemba, ilimkamata daktari huyo akituhumiwa kuomba rushwa ya ngono kwa mgonjwa wake kama malipo ya huduma ya uchunguzi wa Ultra Sound.

Ruvu Shooting ya  Masau Bwire yamlilia Ibrahim Akilimali
Ibrahim Akilimali aaga dunia, kuzikwa kesho Tandale kwa Mtogole