Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ipo tayari kuwakaribisha wawekezaji wa Mafuta na Gesi Asilia ili kuendeleza shughuli za utafiti na uchimbaji.

Dkt. Mwinyi, ameyasema hayo leo Agosti 10, 2022 katika hafla ya makabidhiano ya ‘Data’ za utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwa vitalu vya Zanzibar ambayo imefanyika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

Makabidhiano ya ‘Data’ za utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwa vitalu vya Zanzibar ambayo imefanyika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

Makabidhiano hayo, yamefanyika baina ya Waziri wa Nishati, January Makamba wa Tanzania Bara na Waziri wa Uchumi wa Buluu Suleiman Masoud Makame wa Tanzania Visiwani mbele ya Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi.

Data hizo, ambazo zimehifadhiwa katika mfumo wa kielektroniki, nakala ngumu, sampuli za miamba na kikemikali ambapo Rais Mwinyi amesema hatua ya kupokea data hizo ni mwanzo wa kuongeza jitihada za kukuza sekta ya mafuta na gesi asilia.

Ujenzi Bwawa la kufua umeme la Nyerere bado asilimia 33
Simba SC kushiriki CAF SUPER LEAGUE