Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ina dhamira ya dhati kuhakikisha usalama wa Wananchi kwa kulinda afya zao kupitia hatua stahiki za kupima ubora wa bidhaa mbalimbali, zinazotumika nchini.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Machi 15, 2023 katika Ofisi za Taasisi ya Viwango Zanzibar – ZBS, zilizopo Mkoa wa Mjini Magharibi wakati wa ufunguzi wa maabara mpya nne za kisasa.

Rais Mwinyi akipokea maelekezo katika maabara hiyo.

Amesema, “hatua hii inafungua ukurasa mpya wa maendeleo katika suala la uchunguzi wa ubora wa bidhaa Zanzibar kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.”

Maabara hizo mpya nne za kisasa za Taasisi hiyo yaZBS, ni pamoja na Maabara ya Vimelea, Vifungashio, Nguo na Ngozi pamoja na Umeme.

Wakimbizi 3000 wa Kongo waomba hifadhi Tanzania
Madaktari Bingwa wapiga kambi, waanza upasuaji Tabora