Chama cha Judo Zanzibar kinatarajia kuwa mwenyeji kuandaa mashindano ya  11 ya Judo ya Afrika Mashariki na Kati ambayo yanatarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka 2017.

Taarifa hiyo rasmi imetolewa leo na Makamu wa rais wa shirikisho la Judo Afrika Mashariki na Kati, Yussuf Thabit Mbalambula alipozungumza na waandishi wa habari.

Mbalambula amesema baada ya kufanya kikao chao kwenye shirikisho lao wameamua mashindano hayo yafanyike Zanzibar mwakani baada ya mwaka huu kufanyika Bunjumbura Burundi hivi karibuni ambapo wenyeji Burundi walishinda nafasi ya kwanza na Zanzibar ikashinda nafasi ya pili.

“Baada ya kukutana shirikisho letu, tumeamua mwakani Zanzibar awe mwenyeji wa mashindano hayo. Mashindano yatafanyika kabla ya mwezi Machi mwakani”. Alisema Mbalambula.

Katika mashindano 10 yaliopita, Zanzibar imewahi kuwa mwenyeji mwaka 2008 na 2013. Hivyo, mwaka ujao, itakuwa ni mwaka wa tatu kwa Zanzibar kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa ya Judo Afrika Mashariki na Kati.

Madiwani Ukawa wavamia ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji Dar
Bomu lalipuka Maskani ya CCM Zanzibar, polisi waanza uchunguzi