Timu ya soka ya wanawake ya Zanzibar imepoteza mchezo wake wa pili katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge) baada ya kufungwa mabao 9-0 na wenyeji Uganda leo mjini Jinja.

Zanzibar iliyofungwa 10-1 na Burundi katika mchezo wa kwanza wa Kundi A, sasa itakamilsha michezo yake ya kundi hilo kwa kumenyana na Kenya keshokutwa wakati imekwishaaga mashindano hayo.

Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens keshokutwa itacheza mchezo wa ke ya mwisho ya Kundi B dhidi ya Ethiopia mjini Jinja.

Kilimanjaro Queens itahitaji ushindi Ijumaa ili tu kuongoza Kundi B na kupata mpinzani tahfifu kidogo katika Nusu Fainali.

Hiyo inatokana na kwamba, Kilimanjaro Queens juzi ilijihakikishia kufuzu Nusu Fainali ya michuano hiyo baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Rwanda.

Mabao ya Kili Queens inayofundishwa na Sebastian Nkoma, yalifungwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika za 11 na 65 na Stumai Abdallah dakika ya 28, wakati ya Rwanda yamefungwa na Ibangarrue Marie na Amina Ally wa Tanzania Bara aliyejifunga.  Rwanda na Ethiopia zitakamilisha mechi za Kundi B kwa kumenyanaa na leo.

Nusu Fainali zitafuatia Septemba 18, kabla ya fainali kufanyika Septemba 20, 2016 ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.

Mrema Awapongeza Ukawa
Ronaldinho Gaucho Kuachana Na Soka