Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amesena Serikali imeweka utaratibu na mazingira bora yatakayosaidia kuhamasisha na kukuza uwekezaji wa wageni na wenyenyi, ili kuchangia ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa zima kwa ujumla.

Mwinyi, ameyasema hayo hii leo Septemba 28, 2022 mjini Zanzibar, katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Msoud Othman kwenye ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Nchi ya Italy na Zanzibar.

Amesema, mazingira bora ya kibishara na uwekezaji yatasaidia kukuza upatikanaji wa ajira kwa wananchi kwa kuhusisha utekelezaji wa mpango wa Maendeleo wa Zanzibar wa 2050, kupitia mashirika ya kikanda na Kimataifa ikiwemo kuhamasisha na kukuza uwekezaji wa wageni na wenyenyi kiuchumi.

“Zanzibar imefungua milango ya kibiashara kwa masharti nafuu ya uwekezaji kupitia jitihada za kuleta mabadiliko ya kiuchumi ili kuleta ufanisi wa kimaendeleo nchini kwa manufaa ya wananchi wake na kuwataka wawekezaji kutosita kutumia fursa zilizpo kuja kuwekeza Zanzibar,” amesema Rais Mwinyi.

kwa kipindi kisichozidi miaka miwili, kuanzia Novemba 2020 kiasi cha miradi 136 imesajiliwa Zanzibar nyenye thamani ya Dola za marekani 1.4 bilioni ambayo pia imechangia ajira za moja kwa moja za vijana zaidi ya elfu 9 huku Serikali ikitarajia kuzifanyia mapitio sera zinazohusina na masuala ya uwekezaji, biashara na uchumi.

Awali, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Uwekezaji Mudrik Ramadhani Soraga amesema kwamba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na jitihada kubwa kutengeneza mazingira bora ya kibiashara na uwekezaji na kwamba hatua hiyo ni muhimu katika kuwashajiisha wafanyabiashara mbali mbali kuja Zanzibar.

Watano wasimamishwa kazi kwa ubadhirifu
Waandamana kulipongeza Jeshi la Polisi