Mfanyabiashara na mama wa watoto wawili wa msanii Diamond Platnumz Zari The Bosslady amewasili nchini Tanzania, leo jioni  Septemba 13, akitokea nchini Afrika Kusini kwaajili ya kuzindua duka jipya la bidhaa za nguo, Danube lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Zari ametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa bila mtoto wake mdogo Nillan kitendo ambacho kimeonyesha huwenda mrembo huyo hajafika kwa ajili ya mpenzi wake na ni kwa muda mchache

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kuwasili, Zari amesema amekuja nchini kwa ajili ya uzinduzi wa duka la Danube na si kitu kingine

“Nimekuja Tanzania kama balozi wa Danube. Kwahiyo nashukuru kwa upendo wetu, na tuendelee kutumia bidhaa za Danube,” amesema Zari.

Zari amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Mlimani City siku ya kesho kwa ajili ya uzinduzi wa duka hilo. Wawili hao waliingia kwenye mgogoro mzito wa mapenzi baada ya mpenzi wake kuchepuka na mwanamitindo, Hamisa Mobetto na kuzaa naye mtoto mmoja.

Juan Mata afanya jambo kubwa kwa watoto maskini
Video: Mpina aagiza kuuzwa kwa ngo'mbe waliokamatwa

Comments

comments