Zarina Hassan aliyewahi kuwa mpenzi wa msanii mkubwa nchini, Naseeb Adbul maarufu kama Diamond Platinumz amefunguka na kuwashauri wanaume wanaochepuka kutumia condom pindi wanaposhiriki tendo na michepuko yao.

Amesema kuwa kwa kufanya hivyo itawasaidia sio tu kupata watoto nje ya mpango bali hata kujizuia na magonjwa ya maambukizi ya Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa na kumuambukiza mtu wako anayekusibiri nyumbani.

”Siwezi sema chepuka mara nyingi kama unavyotaka. Siwezi kusema hivyo, lakini kama ukifanya jaribu kutumia Condom, jaribu kutumia Condom sababu sio tu hautaleta watoto wasiotakiwa, unaweza kupata ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa na sio hivyo tu, utaishia kumletea mtu mwingine ambaye yupo nyumbani anakusubiri urudi nyumbani” amesema Zarina.

Amesisitiza kwa wote wanaofanya hivyo wawafikirie watoto wao kwani endapo wazazi wote wawili wakaugua amehoji ni nani atakayelea watoto, hivyo amesema hata kama jambo hilo linafanywa kwa starehe ni vyema kutumia kinga ili kujikinga na maambukizi ya mgonjwa ya zinaa.

Zari amefunguka hayo moja kwa moja akiwa anazungumzia uhusiano wake na baba watoto wake ambaye waliachana mara baada ya kuchepuka na kuzaa na mwanamke mwingine ambaye ni mwanamitindo nchini Tanzania Hamissa Mobeto.

Aidha Zari amekiri kuwa ni kweli alimpemda sana Diamond ila kilichomshinda ni dharau za hadharani ambazo Diamond alikuwa anamfanyia na amedai kuwa Diamond hakuwa mfano mzuri kwa watoto wake wa kiume ambao kwani siku zote yeye amekuwa akiwafundisha watoto wake kuwaheshimu wanawake lakini alichokuwa anafanya Diamond ni sawa na udhalilishaji ndio maana aliamua kusonga mbele na kuachana na nguli huyo wa muziki nchini.

Serikali kulipasua kati jimbo la Mbagala
Bakayoko atoa ya moyoni kuhusu Conte

Comments

comments