Zari the Bosslady ambae ni mzazi mwenzie na msanii wa bongo fleva Diamond Plutnumz amempongeza Tanasha Donna kwa kupewa ujauzito na msanii huyo lakini pia amemsikitikia mrembo huyo wa Kenya kwa kuwa amepewa ujauzito na baba wa watoto watatu.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Zari  amesema kuwa Tanasha amepewa ujauzito na baba asiyejali watoto wake na kumuita “deadbeat”.

Ameongea kuwa siyo vibaya kubeba mimba ila achukuwe tahadhari kwani amebeba mimba ya baba asiye wajibika kama baba yani “deadbeat father” na ni baba wa watoto watatu.

“natumaini kuwa utakuwa na fedha za kutosha benki kumuhudumia mtoto huyo unajua ni kwasababu yupo hivyo alivyo” alisema Zari kupitia “instalive” yake akiwa Nchini Kenya kwenye mualiko wa Akothee.

Wakati zari akizungumza hayo Diamond na Tanasha walikuwa bize wakipigapicha “photoshoot” kwaajili ya maandalizi ya shughuli ya kifamilia iliyopangwa kufanyika siku ya sabasaba.

LIVE: Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT)
Mgogoro wa China na Marekani waanza kupoa, Trump aruhusu bidhaa za Huawei Marekani

Comments

comments