Mfanyabiashara Zarinah Hassan amesema katika wanaume wote aliowahi kuwa nao katika mahusiano baba Tiffah, maarufu kama Diamond Platinumz ni mwanaume ambaye alikuwa hana pesa kulinganisha na wanaume wengine ambao amewahi kuwa nao.

Amesema hayo kupitia ukurasa wake wa instagram wakati akiwajibu baadhi ya mashabiki wake waliomuhoji kuwa endapo Diamond asingekuwa tajiri na maarufu Zari asingeweza kuwa naye kimahusiano.

“Siongei haya ili kuonekana na roho mbaya lakini nimeshawahi kuwa na wanaume wenye pesa nyingi na yeye hayupo kwenye hao watu kwahiyo sikuwa naye kwa ajili ya pesa na umaarufu , wanaume zangu wote niliowahi tembea nao ni matajiri lakini sijapata ambaye hatakuwa anabadilisha wanawake”. Amesema Zari.

Zari amesema hayo kufuatia sakata la aliyekuwa mchumba wake kumzalisha mwanamke mwingine mbali ya kwamba nayeye tayari alikuwa amezalishwa watoto wawili.

Imekuwa ni tabia ya wanaume wengi kutokuridhika na mwanamke mmoja na hii ndio sababu hata ndoa nyingi kuvunjika kutokana na tabia ya wanaume kuchepuka kimahusiano au kuleta watoto nje ya ndoa.

Aidha mara baada ya penzi la wawili hao kuvunjika bado za chini ya kapeti hazivuja kuonesha mwanamke huyu tajiri nchini Uganda, Zari yupo kimahusiano au hayupo kimahusiano kwani bado hajaweka wazi jambo hilo, huku Diamond Platinumz tayari ameweka wazi mahusiano yake na mtangazaji kutoka Kenya, Tanasha Dona ambapo wametangaza ndoa yao kufanyika hivi karibuni huku wasanii wakubwa duniani wakitajwa kuhudhuria ndoa hiyo.

 

 

 

 

Trump atoa mpya kuhusu Kim Jong Un, kukutana Vietnam
Video: Trailer filamu ya kwanza kuoneshwa Netflix ya Wema, Aunt Ezekiel na Van Vicker

Comments

comments