Kufuatia video ya wimbo wa msanii wa bongo fleva nchini Diamond kutoka akiwa amemshirikisha Rayvany na kibao chao cha Iyena kumekuwa na mvumo wa maneno mengi yakidai kuwa kuonekana kwa Zarinah Hassan katika video hiyo kumedhihirisha wazi kuwa wawili hao wamerudiana.

Zari kupitia ukurasa wake wa instagram ameamua kuzima mvumo huo kwa kuweka wazi kuwa uhusiano uliopo kati yake na baba watoto wake, Diamond Platinumz ni kama wazazi tu na si vinginevyo.

Amesema wameamua kufanya hivyo kwa ajili ya watoto wao hivyo mashabiki wao waelewa hivyo na kwamba wanawapenda sana.

”Just to clear the air, we are not back together but have agreed on co-parenting as per my break up post that will remain great parents to our lovely kids. Just a lil note to all our fans. We love you too.

Aidha Zari ameamua kusema hayo kufuatia tetesi zilizovuma hivi karibuni zikidai kuwa wawili hao wamerudisha penzi lao lililovunjika mwaka huu katika siku ya wapendanao ya Valentine ambapo Zari alivunja utaratibu wa siku hiyo ambayo wapenzi hutumiana maua mekundu kama ishara ya upendo yeye alituma ujumbe mzito uliosindikizwa na ua jeusi, ua lililozua gumzo mtandaoni.

Magazeti ya Tanzania leo Juni 12, 2018
Diamond athibitisha kumnunulia Hamisa ghorofa