Mfanyabiashara maarufu nchini Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe mzito uliosomeka kumlenga mwanamitindo Hamisa Mobeto juu ya wakati mguu anaoupitia.

Zari kupitia ukurasa wake wa Instagram amemtaka Hamisa kusonga mbele bila kugeuka nyuma na hana haja ya kujielezea kwa mtu yeyote juu ya jambo lolote kwani hii ni safari ya maisha yake hivyo hakuna anayehitaji kuelewa zaidi yake.

Hivyo amemtumia salamu za upendo na kumwambia afute machozi na kuyaweka mambo yake sawa.

”Never give anyone the power to choose between you and someone else. If they cant decide, decide for them. Walk tf away and never look back. Go where your celebrated. Dont even explain it to anyone your journey is yours. no body has to understand it but you. Sending nothing but love to you sis TZ  now wipe those tears and fix that”

Akimaanisha; Usimpe mtu mamlaka ya kuchagua kati yako na mtu mwingine, Kama hawawezi kuchagua, mchagulie. Songa mbele usiangalie nyuma, nenda utakofurahia, Huna sababu ya kumueleza kila mtu, maisha ni safari yako hakuna mtu anahitaji kuelewa zaidi yako. Natuma salamu za upendo kwako dada huko Tanzania, sasa futa machozi na weka mambo sawa” ujumbe wa Zari unasomeka hivyo kwa tafsiri ya kiswahili.

Aidha Zari na Hamisa wamekuwa hawana mahusiano mazuri kutokana na Diamond kuwachanganya kimapenzi, hivyo ujumbe huo umewashtua mashabiki wingi upande wa Zari na Hamisa kwani Zari ameonesha kukua kwa kiasi kikubwa na hana uhasama na Hamisa, japo siku za nyuma wawili hao wamekuwa wakirushiana maneno ya kejeli.

Ujumbe huo wa Zari wa kumtia nguvu Hamisaa umekuja kufuatia wakati mgumu anaopitia Hamisa kufuatia kuvuja kwa sauti yake iliyorekodiwa ikidai kuwa anaongea na mganga kuloga familia ya Diamond na Diamond mwenyewe.

Kocha Tite amkabidhi kitambaa Neymar
Live: Rais Magufuli akihutubia wananchi wa Tarime muda huu

Comments

comments