Mrembo kutoka Uganda ambaye hivi sasa ni mama mtoto wa Diamond Platinumz, Zarina Hassan maarufu kama Zari The Boss Lady, amedai kuwa wanamuandaa mtoto wao Tiffah kuwa rais ajaye.

Zari ameeleza kuwa ingawa mwanae amekuwa akipokea matusi tangu hajazaliwa na hata baada ya kuzaliwa, anatumia mapito hayo magumu kutengeneza Himaya na atakuwa rais kama alivyo rais wa sasa wa Liberia, Bi. Ellen Jonson Sirleaf.

Zari na Tiffah

Kupitia Instagram, Zari ameandika ujumbe wake kwa lugha ya kiingereza:

“Matusi from day one even before she was born. “But she is here and strong enough to handle. Boss ladies use bricks thrown at them to build empires. And this right here is my future president in the making #IronLady #EllenJohnsonSirleaf #Kichuna @princess_tiffah.”

Serikali Yazidi Kuwabana Watumishi Watakaofanya Makosa
Zanzibar Ngoma Nzito, Serikali Yatangaza Bajeti ya Uchaguzi wa Marudio