Kituo cha Afya Bugisi Kata ya Didia, Wilaya ya Shinyanga Vijijini kimeanzisha kampeni ya kutoa zawadi ya nguo aina ya Khanga ambazo hutolewa kwa wajawazito wanaokwenda kujifungua kwenye kituo hicho, ambapo zawadi hiyo imetajwa kuwa ni moja ya njia ambayo imekuwa ikisaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Awali idadi kubwa ya wanawake katika kijiji hicho walikuwa wakijifungua majumbani, hivyo kupoteza maisha lakini baada ya kuanza kutolewa zawadi ya khanga kwa wajawazito kwenye kituo hicho wengi wameanza kwenda kujifungulia hospitalini hapo.

Aidha, Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho, Dkt. Zakayo William alithibitisha hayo wakati akipokea zawadi za khanga na msaada wa dawa za kuongeza vitamin kwa wajawazito, kutoka asasi ya kiraia ya Nansy Foundation ya mkoani shinyanga inayo endesha mradi wa kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa Asasi hiyo, Ezra Manjerenga, alieleza kuwa mbali na Khanga pia wamekuwa wakitoa msaada wa dawa za Multipregnacy ambazo zina vitamin nyingi ikiwamo kuongeza damu pamoja na kuwalipia malipo ya Ultrasound ya 5,000 kabla ya kujifungua.

Van der Vaart atundika daruga
Sanamu ya Salah yazua gumzo nchini Misri

Comments

comments