Spika wa Bunge, Job Ndugai amewataka wabunge wa kanda ya Ziwa kuungana kwa pamoja na kusemea madhara ya kemikali ya zebaki inayotumika kuchengulia madini.

Ndugai ametoa wito huo leo Aprili 27, bungeni wakati Bunge likijadili hotuba ya Wizara ya nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira baada ya mchango wa Mbunge wa Viti Maalum Hawa Mchafu ambaye alieleza kuhusu madhara makubwa yatokanayo na zebaki hasa kwa wachimbaji madini.

“Wabunge wa Kanda ya Ziwa lazima muungane kulisemea hili, hali siyo nzuri hii zebaki ina madhara makubwa kwa wananchi wetu, siyo jambo la kufumbia macho,” amesema Ndugai.

Katika mchango wake Hawa amesema hali ya Afya za wanawake wa Kanda ya Ziwa hasa wanaofanya kazi za madini migodini zimekuwa shakani, na kuiomba Serikali kuingilia kati.

Fahamu tabia za kimbunga, sababu za kuyeyuka kwa jobo
GSM wamefanya kazi kubwa sana Yanga, basi tu..