Ofisi ya rais wa Ukraine, imesema Urusi itawajibika kuwalipia wahanga wa njaa ya enzi ya Sovieti iliyosababisha vifo vya mamilioni ya watu katika majira ya baridi kati ya mwaka 1932-1933, pamoja na matendo yake katika vita vya sasa nchini Ukraine.

Mkuu wa utawala kwenye ofisi hiyo ya Rais, Andriy Yermak ameandika kwenye mtandao wa Telegram kuwa, Urusi chini ya Vladmir Putin itawalipa wahanga wote wa Holodomor na kujibu kuhusu uhalifu inaoufanya sasa.

Maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga wa Holodomor. Picha ya Daily Sabah

Andiko hilo, limechapishwa na Yermak ikiwa ni siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga wa Holodomor yanayofanyika hii leo Novemba 26, 2022.

Novemba, 1932 kiongozi wa Kisovieti, Joseph Stalin aliwaruhusu Polisi kukamata nafaka na mifugo katika mashamba ya pamoja ya Waukraine sambamba na mbegu ambazo wangezitumia katika msimu ujao na kusababisha raia wengi kufa kwa njaa.

Serikali yatangaza rasmi vita na Al-Shabaab
Picha: Rais Samia akiwakabidhi zawadi Maafisa Wanafunzi