Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera ametoa siku 7 kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha watu waliohusika na upotevu wa maiti za watoto wawili wachanga waliozaliwa wafu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Katavi wanafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Homera ameagiza pia kusimamishwa kwa wasimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti kupisha uchunguzi.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na vikundi vya wajasiriamali wanawake, vijana na walemavu katika Manispaa ya Mpanda kwenye zoezi la ugawaji mikopo kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani.

Kwa Jeshi la Polisi ameagiza kuwafikisha Mahakamani watumishi wa hospitali hiyo, Homera alilihusisha tukio hilo na imani za kishirikina, akiwataka wanasiasa na wadau wa madini kutojihusisha na vitendo hivyo.

Mkurugenzi wa Hospitali, Dkt. Justina Tizeba amesema siku ya tukio, alipokea taarifa June 18 majira ya saa 1:00 jioni akiwa nje ya eneo la kazi, kutoka kwa muuguzi mfawidhi, waliwahoji watendaji katika chumba cha kuhifadhi maiti ambao walikiri kupokea maiti.

Dkt. Tizeba amesema kuwa walitoa taarifa kituo cha Polisi na wahusika walikamatwa na kuwekwa mahabusi, lakini baadaye waliachiwa kwa dhamana.

Tanzania yaongoza mapambano dawa za kulevya duniani
RPC Arusha ahamishwa kituo cha kazi