Timu ya Zesco United kutoka Zambia imezuia mashabiki kuingia uwanja wa Amaan kisiwani Unguja, kuangalia mazoezi ya klabu hiyo baada ya kuamua kufanya mazoezi kwa siri kuelekea mchezo wao kesho kutwa (Jumamosi) dhidi ya wenyeji wao JKU katika Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika.

Mashabiki wa soka visiwani Zanzibar walijitokeza kwa wingi nje ya uwanja wa Amaan wakisubiri timu ya ZESCO ifike uwanjani ili waangalie mazoezi yao, lakini hali ilikuwa tofauti baada ya wachezaji kuingia ndani ya uwanja huo na Mageti yote yakafungwa na hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia.

Baada ya dakika 15 kumaliza mazoezi wakawaruhusu waandishi wa Habari tu pekee yao kwaajili ya kufanya mahojiano na kupiga picha.

Hii ni kawaida hasa katika Mashindano kama haya kwa timu kuzuia mashabiki kwani huwa na wasi wasi kuibiwa baadhi ya mbinu zao pamoja na kujulikanwa kwa haraka wachezaji wao nyota ambao wanaimani waje kuwafunga wenyeji wao.

“ Haturuhusu kuingia uwanjani nyinyi mje Jumamosi kuangalia mechi tu“. Alisema Afisa mmoja wa Zesco.

Mchezo huo utapigwa Jumamosi saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan ambapo siku ya Jumapili muda huo huo kiwanjani hapo watacheza Zimamoto dhidi ya Walaitta Dicha ya Ethiopia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Young Africans na kilio cha kunyimwa uwanja wa taifa
Kamati ya kusimamia ngumi za kulipwa yapewa majukumu