Chama cha Soka visiwani Zanzibar ‘ZFA’ kimepokea kwa mikono miwili taarifa za klabu ya Yanga kumuandikia barua Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar kuomba kuutumia uwanja wa Amaan kwa mashindano mbalimbali ambayo inashiriki ikiwemo ligi kuu Tanzania bara pamoja na mashindano mengine.

Afisa Habari wa ZFA Ali Bakar ‘Cheupe’ amethibitisha kuiona barua hiyo kupitia mitandao mbali mbali ambapo amesema wao kama ZFA hawana matatizo yoyote na wapo tayari hata baadhi ya michezo ya Ligi kuu Zanzibar kuisogeza hadi saa 12 jioni kuipisha Yanga au Yanga kucheza 12 jioni kupisha ligi kuu ya Zanzibar.

Amesema endapo Yanga wakikubaliwa kuutumia uwanja huo wa Amaa,  ZFA inaikaribisha Yanga visiwani Zanzibar.

“Tumeziona taarifa hizo kupitia mitandao mbali mbali, sisi ZFA tunathibitisha barua hiyo tumeiona, na  sisi kama chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar hatuna pingamizi juu ya klabu ya Yanga ambao ni sehemu ya Jamhuri ya Tanzania, sisi tunawambia karibu Zanzibar na tupo pamoja ikiwa watapata ridhaa huko walipoomba,” alisema Cheupe.

Barua hiyo ya Yanga iliyoandikwa na Katibu wao Baraka Deuedit imetumwa moja kwa moja kwa Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar huku nakala ikienda kwa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar ‘ZFA’.

 

Ndanda FC Yapoteza Ajira Ya Rogasian Kaijage
Serengeti boys yawasili nchini kichwa chini